Phyllis Omido

Phyllis Omido (alizaliwa Phyllis Indiatsi Omido 1978 hivi) ni mwanaharakati wa mazingira wa Kenya. Alikuwa mmoja wa watu 6 waliopewa Tuzo ya Mazingira ya Goldman mnamo 2015. Alijulikana kwa kuandaa maandamano dhidi ya kiwanda cha kuyeyusha madini ya risasi kilichoko katikati ya mtaa wa Owino Uhuru, uliopo karibu na Mombasa. Kiwanda hicho kilisababisha sumu ya risasi kwa kuongeza kiwango cha madini ya risasi katika mazingira, kuua wakaazi, haswa watoto, na kuwadhuru wengine, akiwemo mtoto wake mwenyewe. Kiwanda hatimaye kilifungwa.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search